SIASA ZA BONGO BWANA NISHIDA


MAPAMBANO YA KUSAKA MADARAKA MRISHO GAMBO VS GODBLESS LEMA



Image may contain: 1 person, close-up
MRISHO GAMBO
Mrisho Gambo alikuwa katibu wa UV ccm mkoa wa Arusha mwaka 2010 wakati Lema alipochaguliwa kwa Mara ya kwanza kuwa mbunge wa Arusha mjini, mnyukano wa kisiasa kati ya ccm na Chadema uliendelea kuanzia kwenye mgogoro wa umeya lakini baadae Lema akafanikiwa kuwazidi kete na kuibomoa ccm kwa kuwavutia vijana wengi wenye ushawishi ndani ya ccm kuhamia Chadema
Aliyekuwa mwenyekiti wa UV ccm James Ole Milya alihamia chadema na sasa ni mbunge wa Simanjiro
Alphonce Mawazo alijiuzulu udiwani wa Sombetini kwa tiketi ya ccm na kujiunga na Godbless Lema Chadema
Ally Bananga aliyekuwa ccm pia alihama na Alphonce Mawazo na kuhamia Chadema ambapo katika uchaguzi mdogo wa udiwani kuziba nafasi ya Alphonce Mawazo aliyehama chama, Ally Bananga akagombea kwa tiketi ya Chadema na kuchaguliwa kuwa diwani wa Sombetini, hapo Lema akawa amewatimulia vumbi wapinzani wake lakini akiwa amefunguliwa kesi zaidi ya kumi na tano ambazo hajahukumiwa mpaka leo. Gambo akawa hana namna tena na siasa za Arusha bahati take akakumbukwa na Kikwete kwenye uteuzi wa wakuu wa wilaya mwaka 2012 kwa kuteuliwa kuwa mkuu wa wilaya ya Korogwe akimwacha Lema ameshavuliwa ubunge,. Miezi michache baada ya Gambo kuteuliwa Godbless Lema akashinda rufaa yake na kurudishiwa ubunge.. Lema akaendelea kupeta na hatimaye kuifuta kabisa ccm jijini Arusha kwenye uchaguzi mkuu mwaka 2015
Episode 2
Miezi michache baaada ya Lema kuchaguliwa kuwa mbunge wa Arusha mjini tena, Mrisho Gambo akapata uteuzi wa kuwa mkuu wa mkoa wa Arusha,. Hapo ndo akapata nafasi nzuri ya kulipiza kisasi kwa hasimu wake. Gambo alitegemea kunufaika na katazo LA mikutano ya vyama vya siasa lakini Lema aliendelea kufanya kama mbunge., hapo Gambo akakosa njia ya kujiimarisha kisiasa kutokana na umaarufu wa kisiasa wa Lema jijini Arusha,. Ndo maana Siku moja kabla ya Lema kukamatwa, kiongozi wa UV CCM mkoa wa Arusha alilalamika Lema kufanya siasa badala mikutano ya mbunge
Baada ya Lema kuwekwa rumande, Mrisho Gambo amekuwa akieneza chama chake bila upinzani wowote

Image may contain: 1 person, standing

Comments

Popular posts from this blog

Magonjwa 10 Muhimu ya Kupima na Mpenzi wako Kabla ya Kuzaa Mtoto