Magonjwa ya kurithi ni yapi? Haya ni magonjwa ambayo yapo kwenye koo za watu fulani na hurithiwa kutoka kizazi mpaka kizazi lakini pia magonjwa haya huweza kutoka kwa mwanamke na mwanaume ambao kwa macho ni wazima kabisa na kuzaa watoto wenye matatizo ya kiafya. Kwenye jamii zetu za kiafrika ni jambo la kawaida sana kuzaa tu bila kupima kujua kama kuna hatari ya kuzaa mtoto mwenye matatizo makubwa ya kiafya kutokana na vimelea vya kurithi yaani DNA ambazo wazazi husika wamezibeba, mimba nyingi zimekua zikisingiziwa kwamba hazikupangwa na wakati kila mtu anajua mwisho wa ngono zembe bila njia yeyote ya uzazi wa mpango ni mimba. Hii ni tofauti na nchi zilizoendelea ambapo wazazi hupima vipimo hivi kabla ya kuamua kuzaa na hata ikigundulika mtoto anayekuja atakua na matatizo mimba hiyo hutolewa ili kuepusha maumivu ambayo mtoto huyo angeyapata kama angezaliwa na maumivu ya kisaikolojia na kiuchumi ambayo wazazi wanaozaa watoto kama hawa wanayapata, hii ni kwasababu ya k...
Comments